WHO: Covid-19 hausambazwi kupitia kuwanyonyesha watoto

Janga la ugonjwa wa Covid-19 limevuruga pakubwa juhudi za kuhakikisha akina mama wanawayonyesha watoto wao, hali ambayo pia inaweza kuchangia tatizo la utapia mlo na pia kutatiza shughuli za kilimo.

Hayo ni kulingana na shirika la afya duniani WHO pamoja na shirika la watoto duniani la UNICEF.

Kwenye taarifa ya pamoja,mashirika hayo yalisema janga la COVID-19 linatishia kutatiza hatua zilizopigwa katika muda wa miongo minne iliyopita, kuhakikisha kwamba akina mama wanawanyonyesha watoto wao.

Also Read
Maraga ateta kuhusu vipengee vya BBI vinavyohujumu uhuru wa Mahakama

Hayo yanatokana na habari za kupotosha kuwa ugonjwa wa Covid 19 unaweza kuenezwa wakati wa kuwanyonyesha watoto.

Shirika la WHO limekariri kuwa hakuna ushahidi wowote kubaini kuwa ugonjwa huo unaweza kusambazwa kupitia unyonyeshaji watoto.

Kwa hivyo akina mama wameshauriwa kuendelea kuwanyonyesha watoto wao kwa vile ni moja wapo wa njia za kuimarisha afya ya watoto.

Also Read
Mifumo hafifu ya sheria yalaumiwa kwa ongezeko la dhuluma za kimapenzi kwa watoto

Hatua hiyo pia huwakinga watoto dhidi ya maambukizi ya maradhi ya kawaida miongoni mwa watoto.

Wiki ya kuadhimisha  unyonyeshaji, huadhimishwa duniani kati ya tarehe moja na tarehe saba mwezi huu kila mwaka ili kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kumnyonyesha mtoto.

Katika mahojiano na runinga ya shirika la In KBC, Rose Wambu kutoka wizara ya elimu kitengo cha lishe, alisema kina mama wote wanapaswa kuwa na habari kuhusu unyonyeshaji kwa kuwa huwa inaboresha uhusiano katika ya mama na mtoto.

Also Read
Waziri mkuu wa Tanzania asema Rais Magufuli anachapa kazi afisini mwake

Kwa Mujibu wa Wambu, unyonyeshaji husaidia mwili wa mtoto kuwa na Kinga na humsaidia mama kurejelea hali yake ya kawaida kwa haraka.

  

Latest posts

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

COVID-19 yavuruga mbinu za upangaji uzazi hapa nchini

Tom Mathinji

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi