Mkuu wa shirika la afya duniani-WHO amesema kuwa ana matumaini kuwa janga la virusi vya corona litakabiliwa ipasavyo mwaka huu mpya wa 2022 mradi tu mataifa yashirikiane kudhibiti kusambaa kwake.
Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus alionya dhidi ya mikakati isiyofaa ya kujaribu kudhibiti janga hilo kama kuficha chanjo na kukosa kushirikiana ipasavyo kwa mataifa mbalimbali.
Matamshi yake yanawadia miaka miwili tangu shirika hilo la WHO kuarifiwa kuhusu visa vya virusi hivyo vinavyokaribia kufanana na ugonjwa wa pneumonia nchini China.
Visa vilivyodhibitishwa duniani vya virusi hivyo ni milioni 287 huku watu wapatao milioni 5.5 wakifariki.
Sherehe za kukaribisha mwaka mpya zilikosa misisimuko ya kawaida baada ya mataifa kadhaa kupiga maarufuku mikusanyiko ya watu.
Nchini Afrika kusini ambako kisa cha kwanza cha Covid-19 aina ya Omicron kiliripotiwa, marufuku ya wakati wa usiku sasa yameondolewa.
Mataifa kadhaa yakiwemo Uingereza, Ugiriki na Italia, yaliripoti visa vya Omicron, hatua iliyosababisha safari nyingi za ndege kusitishwa ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.