WHO yahimiza raia kuvaa barakoa wakati wa sherehe za Krismasi

Shirika la Afya Duniani, WHO, limehimiza raia wa Bara Ulaya kuvalia barakoa kwenye mikusanyiko ya familia wakati wa msimu wa siku kuu ya Krismasi.

Taarifa kutoka afisi ya shirika la WHO Barani Ulaya imesema kuongezeka kwa mikutano ya familia na marafiki kote Barani Ulaya wakati wa siku kuu ya msimu wa baridi kunasababisha hatari kubwa ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19.

Also Read
Uchaguzi mkuu nchini Iran wavutia Idadi ndogo ya wapiga kura

Taarifa hiyo imesema Bara Ulaya limo kwenye hatari kubwa ya wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya Corona mapema mwaka ujao kwani maambukizi ya virusi hivyo yanaongezeka.

Also Read
Jimbo la Texas nchini Marekani kuondoa agizo la uvaaji barakoa

Mataifa katika bara hilo yamekuwa yakinakili maelfu ya visa vipya vya maambukizi na mamia ya vifo.

Ujerumani ilikuwa miongoni mwa nchi zilizoimarisha masharti leo na kufunga shule na biashara zisizo muhimu.

Also Read
Uingereza na Russia mbioni kuimarisha chanjo dhidi ya Covid-19

Wakati uo huo, Rais wa Tume ya Bara Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema chanjo ya kwanza ya ugonjwa wa COVID-19 itaanza kutumika katika muda wa wiki moja.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi