William Ruto achaguliwa Rais wa Tano wa Kenya

William Samoei Ruto ndiye Rais wa tano wa taifa hili baada ya kuzoa kura 7,176141.

William. Ruto aliyewania wadhifa huo kwa tiketi ya Muungano wa Kenya Kwanza, alimshinda mpinzani wake wa karibu Raila Odinga wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga aliyepata kura 6.942930.

Also Read
Halfa ya uzinduzi wa ripoti ya BBI yang’oa nanga Bomas

Kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoyah alikuwa wa tatu kwa kupata kura 61,969, huku mwaniaji wa Urais kwa tiketi ya chama cha Agano Waihiga Mwaure akishikilia nafasi ya nne.

Akitangaza matokeo hayo katika kituo cha kujumlisha kura za kitaifa kilichoko ukumbi wa Bomas Jijini Nairobi, mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, alisema mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulikuwa wenye uadilifu na ulizingatia sheria kikamilifu.

Also Read
Rais Kenyatta apongeza uhusiano baina ya Kenya na Hungary

Kulingana na Chebukati, William Ruto alipata asilimia asilimia 25 katika kaunti 39, huku Raila Odinga akipata asilimia 25 katika kaunti 34.

Also Read
Baadhi ya wabunge wa Mlima Kenya waanzisha mashauriano ya kumuunga mkono Ruto

Aidha Waihiga Mwaure na George Wajackoyah hawakufikisha asilimia 25 katika kaunti yoyote.

Jumla ya wakenya Milioni 14, walishiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022, kati ya wapiga kura milioni 22 waliosajiliwa.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi