Wimbo mpya wa Bahati wapata ufuasi wa watu milioni moja

Mwanamuziki wa hapa nchini ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha ubunge cha Mathare, hatimaye amepata ufuasi wa watu milioni moja  katika wimbo wake mpya.

Bahati sasa anajiunga na Mwanamuziki mwenzake Otile Brown ambaye ana ufuasi wa mashabiki milioni 1.15.

Also Read
Father Weezdom!

Hatua hiyo mpya imeafikiwa baada ya kuzindua wimbo mpya “Sweet Love” ambayo amemshirikisha mke wake na mwimbaj Diana B.

Also Read
Otile Brown asajili msanii kwenye kampuni yake ya muziki

Wimbo huo wa “Sweet Love” unaelezea mapenzi ya wanandoa, pamoja na changamoto za ndoa.

Hata hivyo Bahati na mke wake wanaingia katika ukurasa mpya, kwani Mwanamuziki huyo tajika anawania wadhifa wa ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Also Read
Wasanii Ringtone, Bahati, Mr. Seed na Dk Waungana Kumfariji David Mulei

Bahati alikabidhiwa tiketi ya kuwania wadhifa huo na Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni, katika makao makuu ya chama hicho.

  

Latest posts

Msanii Kajala Masanja amsamehe Harmonize

Tom Mathinji

Tarrus Riley awasili nchini kwa tamasha la Koroga Festival

Tom Mathinji

Diamond Ajisifia Kuwa Mwanamuziki Bora Tanzania

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi