Wito watolewa wa kubuniwa kwa afisi zaidi za usajili wa watu Garissa

Shirika moja la kutetea haki za kibnadamu  kwa jina  Haki Na Sheria, linataka kubuniwa  kwa afisi za kusajili watu nje ya mji wa  Garissa  ili kuwapunguzia wakazi mwendo mrefu na fedha.

Mwenywekiti  wa shirika hilo tawi la Garissa Haretho Bulle, alisema wakazi wa sehemu hiyo hulazimika kusafiri kilomita  kadhaa ili kutafuta huduma za usajili.

Also Read
Zoezi la kuchanja mifugo kwa wingi lang’oa nanga Garissa

Kulingana na  Bulle wale wanaotafuta vyeti vya usajili ni pamoja na watu wakongwe ambao hawakupata huduma hiyo.

Muhamed Ahmed ambaye ni mkazi na pia mzee wa eneo hilo alisema wamekuwa wakilazimika kutembea mwendo mrefu kwa afisi za usajili wa watu kutafuta huduma hizo ambazo wakati mwingine hazikupatikana.

Also Read
Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

“Serikali imesema watoto lazima wawe na vyeti vya kuzaliwa ili wasajiliwe shuleni, lakini tuna changamoto kadhaa za kupata vyeti hivyo. Hatua zinapaswa kuchukuliwa kuhakikisha huduma hizi zinarahisishwa,” alisema Ahmed.

Bulle alitoa wito kwa wakazi hao kuwasijili watoto wakati ufao  na kuhakikisha watoto wao wanapata huduma  kama vile vitambulisho vya kitaifa  pamoja na vyeti vya usafiri siku za usoni .

Also Read
Washukiwa watatu wa ugaidi wanaswa kaunti ya Garissa

Katika kaunti ya Garissa, ni eneo la Masalani na Garissa mjini ambayo yana afisi za usajili wa watu. Afisi ya Balambala iliyofunguliwa hivi majuzi ilifungwa baadaye kutokana na ukosefu wa wafanyikazi wa kutosha.

 

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi