Wizara ya Afya yanakili visa 132 vya maambukizi ya COVID-19

Wizara ya Afya humu nchini imenakili visa 132 vya maambukizi ya virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli 4,220 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii imefikisha idadi jumla ya maambukizi ya virusi hivyo nchini kuwa 102,353 huku jumla ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,228,047.

Also Read
Mwaniaji urais wa Congo-Brazzaville afariki kutokana na Covid-19

Kati ya visa hivyo vipya vya maambukizi, 111 walikuwa wakenya huku 21 wakiwa raia wa kigeni.

Visa 70 ni vya wanaume ilhali 62 ni vya wanawake, wote wa kati ya umri wa miaka 11 hadi 96.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 96, Kiambu 8, Taita Taveta 6, Kisumu 4, Nakuru 4, Meru 3, Kilifi 2, Mombasa 2, Uasin Gishu 2, Embu 1, Garissa 1, Machakos 1, Kajiado 1 na Kericho 1.

Also Read
COVID-19: Visa vingine 331 vyathibitishwa Kenya, wagonjwa 3 wafariki

Wagonjwa 62 wamepona kutokana na virusi hivyo, 45 walitoka katika mpango wa kuwashughulikia wagonjwa nyumbani huku 17 wakipona kutoka hospitali mbali mbali nchini.

Also Read
Rais Kenyatta akutana na maafisa wakuu Serikalini

Idadi jumla ya waliopona sasa ni watu 84,790.

Hata hivyo, wagonjwa watatu zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa 1,794.

Kwa sasa wagonjwa 360 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku wagonjwa 1,292 wakishughulikiwa katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi