Wizara ya Afya yanakili visa 394 vya COVID-19 na vifo 14

Wizara ya Afya humu nchini imenakili visa vipya 394 vya maambukizi ya virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli 2,923 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii imefikisha idadi jumla ya maambukizi ya virusi hivyo nchini kuwa 139,842 huku jumla ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,523,313.

Kati ya visa hivyo vipya vya maambukizi, 374 walikuwa Wakenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni.

Also Read
Mfungwa afariki kutokana na Covid-19 akiwa korokoroni Migori

Visa 209 ni vya wanaume ilhali 185 ni vya wanawake, wote wa kati ya umri wa miezi minane hadi miaka 95.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza kwa idadi kubwa zaidi ya maambukizi 246, ikifuatwa na Kiambu kwa visa 29, Machakos 23, Uasin Gishu 22, Kitui 20, Nakuru 15, Kajiado 10, Kilifi 10, Trans Nzoia 5, Mombasa 4, Murang’a 3, Makueni 2, Nandi 1, Taita Taveta 1, West Pokot 1, Elgeyo Marakwet 1 na Embu 1.

Also Read
COVID-19: Maambukizi yapanda zaidi siku moja kabla hotuba ya Rais

Wagonjwa 2,217 wamepona kutokana na virusi hivyo, 675 walitoka katika mpango wa kuwashughulikia wagonjwa nyumbani huku 1,542 wakipona kutoka hospitali mbali mbali nchini. Idadi jumla ya waliopona sasa ni watu 96,578.

Also Read
Kituo cha utafiti wa ugonjwa wa Saratani chazinduliwa hapa nchini

Hata hivyo, wagonjwa 14 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa 2,258.

Kwa sasa wagonjwa 1,576 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku wagonjwa 6,182 wakishughulikiwa katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi