Wizara ya Afya yaripoti visa vipya 1,065 vya Corona

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona humu nchini imezidi kuongezeka baada ya watu wengine 1,065 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Hii ni baada ya Wizara ya Afya kufanyia uchunguzi sampuli 7,386 na kufikisha jumla ya sampuli zilizopimwa humu nchini hadi 737,749.

Jumla ya maambukizi ya virusi hivyo sasa imefikia 61,769 tangu kisa cha kwanza kuripotiwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Also Read
COVID-19: Kenya yaripoti visa vipya 366 huku mgonjwa mmoja akiaga dunia

Kati ya visa hivyo vipya, 993 ni vya Wakenya ilihali 72 ni vya raia wa nchi za kigeni.

661 kati ya walioambukizwa ni wanaume huku wanawake wakiwa 404, kati ya umri wa miaka mitatu hadi 104.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongozwa baada ya kuripoti visa 263, ikifuatwa na Mombasa kwa visa 181, Uasin Gishu 63, Nakuru 62, Kisumu 53, Kiambu 47, Kajiado 38, Kilifi 36, Kericho 30, Busia 30, Baringo 26, Kakamega 25, Nyeri 21, Turkana 21, Homabay 20, Trans Nzoia 18, Kwale 15, Nyandarua 13, Siaya 13, Nyamira 13, Machakos 12 na Kisii 11.

Also Read
Kenya yaripoti visa vipya 236 vya maambukizi ya COVID-19

Kufikia sasa, jumla ya wagonjwa 1,270 wanapata matibabu katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini huku 5,537 wakiwa kwenye mpango wa kuhudumiwa nyumbani.

Wagonjwa 59 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, huku 26 kati yao wakiwa wanapata usaidizi wa kupumua nao 27 wanapokea hewa ya oksijeni.

Also Read
Visa 147 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa nchini

Aidha, Wizara ya Afya imethibitisha kwamba wagonjwa 888 wamepona kutokana na ugonjwa huo; 824 kati yao wakitoka katika mpango wa kuhudumiwa nyumbani na 64 hospitalini.

Jumla ya waliopona kufikia sasa ni 41,019.

Hata hivyo, wagonjwa 12 wameaga dunia kutokana na makali ya virusi hivyo na kufikisha idadi ya maafa hadi 1,103.

  

Latest posts

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Serikali yaongeza kafyu ya kuto-toka nje usiku katika kaunti tatu za Rift Valley

Tom Mathinji

Karua asema Muungano wa Azimio utahakikisha uongozi bora

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi