Wizara ya Afya yathibitisha maambukizi mapya 153 ya korona

Idadi ya maambukizi ya virusi vya korona humu nchini imeongezeka hadi 101,009 baada ya watu wengine 153 kuambukizwa saa 24 zilizopita.

Wizara ya Afya humu nchini imethibitisha hayo baada ya kufanyia uchunguzi sampuli 3,922 na kufikisha jumla ya sampuli zilizopimwa hadi 1,192,605.

Kati ya waliothibitishwa leo, 123 ni Wakenya ilhali 30 ni raia wa kigeni. Kijinsia, 91 ni wanaume na 62 ni wanawake.

Also Read
Huenda hitaji la kuwataka wabunge na wawakilishi wadi kuwa na digrii likaahirishwa

Mgonjwa mwenye umri mchanga zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na miaka 80.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza  kwa kuripoti idadi kubwa zaidi ya maambukizi mapya 93, ikifuatwa na Mombasa iliyoripoti visa 13, Kiambu 8, Nakuru 6, Turkana 5, Kajiado 3, Kisumu 3, Taita Taveta 3, Busia 2, Nandi 2, Trans Nzoia 2, Uasin Gishu 2, Kirinyaga 2, Elgeyo Marakwet 1, Embu 1, Kilifi 1, Machakos 1, Makueni 1, Meru 1, Murang’a 1, Samburu 1 na Siaya 1.

Also Read
Wanawake wanaougua Fistula kunufaika na Matibabu bila malipo katika hospitali ya Kenyatta

Wizara ya Afya pia imethibitisha kupona kwa wagonjwa 54 waliokuwa wakiugua covid-19.

Kati ya hao, 35 walikuwa kwenye mpango wa uangalizi wa nyumbani ilhali 19 wameruhusiwa kuondoka kutoka vituo mbali mbali vya afya nchini.

Kufikia sasa, jumla ya wagonjwa 83,990 wamepona kutokana na ugonjwa huo.

Also Read
COVID-19: Kenya yanakili visa vipya 495 huku wagonjwa 19 wakifariki

Kulingana na taarifa ya wizara hiyo, hakuna maafa yaliyotokea katika muda wa masaa 24 yaliyosababishwa na COVID-19, hivyo idadi ya maafa imesalia 1,766.

Taarifa hiyo pia imesema jumla ya wagonjwa 471 wanahudumiwa katika vituo vya afya ilhali 1,471 wako katika mpango wa kutunzwa nyumbani.

Wagonjwa 27 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 12 kati yao wakitumia vipumulishi huku 15 wakipokea hewa ya ziada ya oksijeni.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi