Wizara ya fedha yapata idhini ya kutoa pesa kwa kaunti ya Nairobi

Kaimu gavana wa Nairobi Benson Mutura ametia saini amri ya gavana ambayo inaipa wizara ya fedha idhini ya kutoa pesa kwa kaunti hiyo.

Hatua hiyo imejiri saa chache baada yake kuapishwa kuwa kaimu gavana kuchukua mahala pa Mike Sonko aliyeondolewa mamlakani kwa misingi ya matumzii mabaya ya mamlaka na ukiukaji wa katiba.

Also Read
Gavana Sonko akanusha shtaka jipya la matumizi mabaya ya mamlaka

Gavana huyo aliyeng’atuliwa alikuwa amekataa kutia saini amri hiyo na hivyo kutatiza utekelezaji shughuli katika kaunti hiyo tangu mwezi oktoba.

Amri hiyo sasa inatoa idhini ya utekelezaji  wa bajeti ya kaunti ya Nairobi katika kipindi cha matumizi ya pesa za serikali cha mwaka 2020-21 ya shilingi bilioni-37.5.

Katika bajeti hiyo halmashauri ya usimamizi wa eneo la jiji la  Nairobi ilitengewa shilingi bilioni 27.1 ambapo aliahidi kushirikiana kwa karibu na halmashauri hiyo kwa minajili ya utoaji huduma bora kwa kaunti hii.

Also Read
Hoteli za watalii zateketea Msambweni kaunti ya Kwale
Also Read
Hatma ya Mike Sonko sasa imo mikononi mwa bunge la Senate

Mara tu pesa hizo zitakapotolewa kwa hazina ya mapato ya kaunti, wafanyikazi wa kaunti na bunge la kaunti hiyo watalipwa mishahara yao.

Mutura atashikilia wadhifa huo wa gavana hadi tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) itakapotekeleza uchaguzi mdogo wa gavana mpya katika muda wa siku 60.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi