Wizara ya nchi za kigeni yataka wakenya kutofanya kazi Saudi Arabia

Baada ya kuagaziwa kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya humu nchini jinsi wakenya wanavyoteseka na hata wengine kufariki katika hali tatanishi nchini Saudi Arabia, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni sasa inashinikiza kusimamishwa kwa muda shughuli za uajiri na usafirishaji wa Wakenya wanaoelekea nchini Saudia Arabia kufanya kazi.

Also Read
Rais Kenyatta na Mama Taifa Margaret Kenyatta wachanjwa dhidi ya Covid-19

Katibu katika wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Macharia Kamau, alipofika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu ajira aliilaumu wizara ya leba na taasisi ya kitaifa ya kuajiri watu kwa kuvuruga shughuli ya kuwaajiri wafanyakazi hao.

Wabunge hatahivyo wamesema hawaridhishwi na sababu iliyotolewa kwenye ripoti hiyo huku wakidai kuwa vifo vya wakenya 41 wanaofanya kazi nchini Saudi Arabia katika kipindi cha miezi tisa iliyopita vilisababishwa na mshtuko wa moyo.

Also Read
Gharama ya Internet nchini Kenya ni ya juu zaidi katika Afrika Mashariki

Balozi Kamau  aliwaambia wabunge kwamba vifo hivyo vingeweza kuepukwa iwapo wizara ya leba ingehakikisha shughuli ya kuwaajiri wafanyakazi raia wa kenya kwenda kufanya kazi katika mataifa ya mashariki ya kati imefanywa kwa uangalifu.

Also Read
Maafisa wote wa kibalozi Jijini Nairobi kuchanjwa dhidi ya Covid-19

Katibu huyo alisema wizara ya mashauri ya kigeni iko tayari kuunga mkono juhudi zozote za kuwalinda wakenya wanaoishi ughaibuni.

Wizara hiyo inataka shughuli hiyo kusimamishwa hadi swala la usalama wa wakenya wanaoenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia lishughulikiwe kikamilifu.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi