Wizkid asema albamu yake mpya imekamilika

Mwanamuziki wa Nigeria Starboy Wizkid, ametangaza kuwa albamu yake ya “More Love Less Ego”  imekamilika na inatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka 2022.

Mwanamuziki huyo wa kupigiwa mfano, alitangaza hayo siku ya Jumapili tarehe 22 mwezi Mei kupitia mtandao wake wa Instagram. Katika tangazo hilo lake, Wizkid aliwashukuru wote waliofankisha kukamilika kwa albamu hiyo.

Also Read
Magawa Atungiwa Wimbo

Mnamo mwaka 2020, Wizkid alizindua albamu yake yake ya nne “Made In Lagos”, amabyo inajumuisha kibao maarufu “Essence” kilichopokea tuzo ya wimbo bora ulimwenguni.

Also Read
Revival Asimulia Maisha Yake

Licha ya kuwa albamu yake “Made In Lagos” kilipata umaarufu mkubwa, Wizkid aliambulia patupu kwani haikupata tuzo yoyote.

Katika wiki zijazo, kunatarajiwa kuwa na ufahamu zaidi kuhusu albamu hiyo inayosubiriwa kwa hamu na ghamu ya  “More Love Less Ego” huku mashabiki na pia wahakiki wake wakisubiri kuona iwapo albamu hiyo itamweesha Wizkid kupata tuzo yake ya kwanza ya kibinafsi ya  Grammy.

  

Latest posts

Msanii Kajala Masanja amsamehe Harmonize

Tom Mathinji

Tarrus Riley awasili nchini kwa tamasha la Koroga Festival

Tom Mathinji

Diamond Ajisifia Kuwa Mwanamuziki Bora Tanzania

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi