Wizkid kushirikiana na mwanamuziki Bella Shmurda

Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kama Wizkid mwanamuziki wa nchi ya Nigeria amekuwa nchini Ghana kwa muda sasa ambapo amekuwa mwenyeji wa wanamuziki wengi kwenye makazi yake nchini Ghana.

Mwanamuziki wa hivi karibuni zaidi kumzuru ni Bella Shmurda wa Nigeria, kulingana na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Video hiyo inamwonyesha Bella Shmurda akiwasili nyumbani kwa Wizkid huku akimwita kwa jina lake “Balogun”.

Also Read
Ada Ameh afiwa na mwanawe wa kipekee

Baadaye tena video nyingine ilichipuza kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha wawili hao wakiwa studioni kurekodi muziki.

Wizkid ni mmoja wa wanamuziki waili wa bara Afrika waliong’ara kwenye tuzo za Grammy baada ya wimbo alioshirikishwa wa Beyonce “Brown Skin Girl” kuibuka mshindi katika kitengo cha video bora ya muziki.

Amekuwa Ghana kwa muda ila hajasema rasmi dhamira yake nchini humo, hata mwezi februari, alitoka Ghana akahudhuria tuzo za Headies awamu ya 14 Jijini Lagos, nchini Nigeria ambapo alishinda tuzo kadhaa kama vile chaguo la watazamaji mwaka 2020.

Also Read
Olu Jacobs, muigizaji mkongwe nchini Nigeria

Mwanamuziki huyu alianza kurekodi muziki akiwa na umri wa miaka 11 pekee katika kundi lake na marafiki wake wa kanisani liitwalo “Glorius Five” na walifanikiwa kutoa albamu moja.

Also Read
Aliyekuwa Rais wa Ghana Jerry John Rawlings amefariki

Alisajiliwa na kampuni ya muziki kwa jina “Empire Mates Entertainment (E.M.E)” mwaka 2009 na kibao kilichompa umaarufu ni “Holla at Your Boy”, ambacho kiko kwenye albamu yake ya kwanza inayoitwa “Superstar” ambayo alizindua mwaka 2011.

Amewahi kushirikiana na wanamuziki wa kimataifa kama vile Drake kwenye kibao kiitwacho “One Dance” ambacho kilifanya vyema katika nchi kadhaa ulimwenguni.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi