Yanga yampiga teke kocha baada ya siku 37

Miamba wa soka nchini Tanzania kilabu ya Yanga wamemtimua kocha wao Zlatko Krmpotic kutoka Serbia baada ya kuwa usukani kwa siku 37 pekee.

Also Read
Nasreddine Nabi wa Tunisia ateuliwa kocha wa YANGA kwa miezi 18

Yanga, walichukua uamuzi wa kumpiga kalamu kocho huyo mapema jumapili siku moja kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchuano wa  ligi kuu.

Also Read
Simba wanyakua ligi kuu ya Tanzania bara kwa mara ya 22

Kocha huyo ambaye awali amezifunza timu za  APR ya Rwanda , Zesco United na  Polokwane City ya Afrika Kusini ndiye meneja wa kwanza kuonyeshwa mlango msimu huu katika ligi kuu ya Tanzania bara.

Also Read
Simba atafunwa mbele ya mashabiki wa nyumbani

Chini ya Krmpotic yanga wamecheza mechi 5 kushinda nne na kutoka sare moja.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi