Mwanamuziki wa mtindo wa rap nchini Marekani kwa jina Ye’ ana imani kwamba Mungu atasaidia kumrejeshea ndoa yake na Kim Kardashian ambayo ilisambaratika.
Mwanamuziki huyo ambaye awali alifahamika kama Kanye West anasema ikiwa hilo litatimia, litasaidia kumotisha wengine wengi ambao ndoa zao zinaelekea Kusambaratika.
Ye aliyasema hayo kwenye L.A. Mission ambapo alikuwa amepeleka msaada wa chakula kwa watu 1,000.
Alisema amewahi kufanya hadharani mambo ambayo hakustahili kufanya kama mume wa mtu lakini anaamini Mungu atasaidia arejelee ndoa yake na Kim.
Mwanamuziki huyo alitaja watoto wake ambao alisema anahitaji kuwa karibu nao na ikiwa hataishi nao kwenye nyumba moja basi atatafuta nyumba iliyo karibu na wanakoishi.
Maneno ya Ye yanajiri siku chache baada ya Kim Kardashian kuonekana akiwa na Pete Davidson huko Santa Monica naye akihusishwa na wanawake wawili ambao ni Irina Shayk na Vinetria.
Kim Kardashian na Kanye West walifunga ndoa mwaka 2014 na wametengana mwaka huu wa 2021 baada ya Kim kuanzisha kesi ya talaka mahakamani mwezi Februari.
Wana watoto wanna ambao ni North West, Psalm West, Saint West na Chicago West.