Zaidi ya watu 100 wafariki kutokana na mafuriko nchini Sudan

Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa-FAO limesema mafuriko makubwa yanayoshuhudiwa nchini Sudan yameathiri takriban thuluthi moja ya ardhi iliyolimwa na familia zipatazo laki-6.

Also Read
Kaunti ya Kilifi yanunua vifaa vya kisasa vya kukabiliana na nzige

Zaidi ya tani milioni moja za nafaka zimeharibiwa hasa mtama ambao ndilo zao kuu na familia nyingi sasa zimelazimika kutumia chakula kidogo kidogo kwa siku.

Also Read
Hatua ya Kenya ya kusitisha uagizaji mahindi yapongezwa na wakulima

Mafuriko hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Mapato yameathiriwa pia huku mimea ya kibiashara ikiwemo migomba ya ndizi na miembe pia ikiathiriwa vibaya.

Also Read
Kenya yailemea Sudan katika mechi ya kirafiki

Shirika la FAO limesema kwamba nzige ambao wameathiri mimea katika eneo hilo la upembe wa Afrika, bado ni tishio kwa nchi hiyo. 

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi