Zakayo kushiriki Kip Keino Classic Continental Tour Jumamosi hii

Bingwa wa bara Afrika katika mbio za mita 5000 Edward Zakayo yuko shwari kushiriki mashindano ya Kip Keino Classic Continental tour Jumamosi hii Septemba 18 baada ya kupona jeraha ambalo limekuwa likimtatiza kwa muda mrefu.

Zakayo aliye na umri wa miaka 19 ,  hajashiriki shindano lolote tangu mwaka  2019 alipojeruhiwa  kiuno .

“Nimeptia wakati mgumu kwa kipindi cha miaka miwili ambayo nimekosa kushirki katika mchezo ninaoupenda kutokana na jeraha,hata hivyo ni fahari yangu kurejea mikiwa tayari kushiriki mashindano ya Kip Keino Classic,imenjichukua muda mrefu kupona jeraha na natumai nitakimbia vizuri “akasema Zakayo

Also Read
Mashindano ya riadha ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 yaanza Kasarani

Zakayo atatimka mbio za mita 5000 Jumamosi hii katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani akipambana na  Jacob Krop,Michael Kibet,Benson Kiplangat,Newton Chruiyot,Levi Kibet,Nicholas Kimeli,Brian Limo,Emmanuel Kiprop,Mike Kiplangat na Godfrey Musanga   wote wa Kenya pamoja na  Isaac Kimeli wa Ubelgiji.

Also Read
Idara ya magereza yawatuza washiriki wake wa Olimpiki

Mashindano hayo yatakuwa ya kitengo cha discretionary ambayo ni  mashindano yanayochaguliwa na chama cha riadha Kenya.

Kip Keino Classic inaaandaliwa kwa mwaka wa pili mtawalia ukiwa mkondo wa 12 na wa mwisho  wa continental tour  nembo ya dhahabu  na yatakuwa ya vitengo vitatu vya National events,Discretionary events na Core events .

Also Read
Mwanariadha bora wa Kenya katika Kip Keino Classic kutuzwa milioni 2 nukta 5.

Kitengo kikuu cha core events kitakuwana fani 10  Pole Vault ,mita 200 ,long jump ,mita 3000 kuruka viunzi na maji ,hammer throw,na mita 100 wanaume na wanawake.

 

 

  

Latest posts

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi