Ziara ya Rais Kenyatta nchini Uingereza kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili

Balozi wa Kenya nchini Uingereza Manoah Esipisu, amesema ziara ya Rais Uhuru Kenyatta katika taifa hilo la bara ulaya, inanuiwa kuimarisha ushirikiano muhimu kati ya nchi hizi mbili.

Akiwahutubia wanahabari Jijini London kabla ya kuwasili kwa Rais Kenyatta, Esipisu alisema kilele cha ziara ya kiongozi wa nchi kitakuwa Rais Kenyatta kuwa mwenyekiti mwenza wa kikao cha kimataifa kuhusu elimu akiwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson.

Also Read
Serikali yajizatiti kuimarisha mifumo ya usafiri na uchukuzi kote nchini

Alisema lengo la kikao hicho kitakachoandaliwa tarehe 28 na 29 mwezi huu ni kukusanya dolla bilioni 5 za kuwekeza kwenye elimu ya mamilioni ya watoto wasiojimudu kote duniani.

Also Read
Shirika la Msalaba Mwekundu latoa misaada kwa waathiriwa wa mafuriko Tana Delta

Alidokeza kuwa wakati wa ziara hiyo, Rais Kenyatta pia atafanya mashauri na waziri mkuu Johnson kuchunguza nyanja nyingine za ushirikiano muhimu baina ya nchi hizi mbili.

Also Read
KRA: Miswada 23 iliyofutiliwa mbali na mahakama haitaathiri ukusanyaji ushuru

Pia kwenye ratiba ya rais itakuwa mashauriano kuhusu ajenda ya Kenya na Uingereza kuhusu mabadiliko ya hali ya anga kwa mkutano ujao wa COPS26 mjini Glasgow.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi