Ziara ya William Ruto nchini Uganda yatibuka

Ziara ya naibu wa Rais William Ruto ya kuelekea nchini Uganda iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumatatu alasiri haikufua dafu.

Ripoti zilidokeza kuwa naibu wa Rais hakupata idhini ya kuondoka nje ya nchi hii kuambatana na kanuni za utumishi wa umma.

Inasemekana naibu huyo wa Rais, aliwasili katika uwanja wa ndege wa Wilson saa nane mchana lakini akashauriwa kutafuta idhini kutoka kwa mkuu wa utumishi wa umma.

Also Read
Wanamuziki wa Nigeria watiwa mbaroni Uganda

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Ruto aliyeashiria tukio hilo alisema ” Nisawa tumwachie Mungu”.

Hata hivyo wizara ya maswala ya ndani ilikanusha madai kwamba ilimzuia naibu Rais kuondoka hapa nchini, ikidokeza kuwa haina mamlaka dhidi ya hatua hiyo.

Also Read
Rais Kenyatta aongoza mazungumzo kati ya wajumbe wa Kenya na wa Somaliland

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara hiyo Nixon Ng’ang’a,  mkuu wa utumishi wa umma ndiye hutekeleza kanuni za utumishi wa umma zinazohitaji watumishi wa umma kupewa idhini ya kusafiri nje ya nchi.

Also Read
Wahudumu wa afya wa kujitolea kaunti ya Embu watishia kusitisha huduma zao

Alisema Waziri wa maswala ya ndani ya nchi hangeweza kwa vyovyote vile kumuidhinisha naibu wa Rais kuondoka.

Mwezi uliopita, naibu wa Rais aliangaziwa sana baada ya ziara yake ya siku mbili nchini Uganda, kuzindua kiwanda cha kutengeneza chanjo akiwa ameandamana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi