Zoezi la ukusanyaji saini lang’oa nanga huku Rais Kenyatta akihimiza Wakenya kuunga mkono BBI

Safari ya marekebisho ya katiba imeanza rasmi Jumatano kufuatia uzinduzi wa shughuli ya ukusanyaji saini kwenye hafla iliyoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo katika Ukumbi wa KICC, Rais Kenyatta amesema mapendekezo ya marekebisho ya katiba kupitia mpango wa BBI ni hatua mwafaka ya kuangazia changamoto ambazo zimekumba taifa hili kwa miaka mingi ikiwemo ujumuishaji kwenye uongozi na usawa kwenye ugavi wa rasilimali.

Kiongozi wa taifa amewahimiza Wakenya kuunga mkono mchakato huo akihoji kwamba marekebisho ya katiba ni hatua mwafaka kwa sababu uhalisia wa Maisha unahitaji mageuzi ya mara kwa mara.

Also Read
Raila: BBI italeta maendeleo kote nchini

“Taifa hili limezaliwa kupitia mageuzi endelevu; ni uzao uliotekelezwa kwa nia. Mti wa taifa hili unanyunyiziwa kupitia mawazo ya mara kwa mara. Bila hivyo, taifa hili litafifia na kufa. Jambo pekee ambalo halibadiliki ni lile lililokufa,” amesema Rais.

Rais Kenyatta amefafanua kwamba mchakato uliopo ni wa kuboresha katiba iliyopo na wala si ya kutafuta katiba mpya.

Also Read
Mswada wa BBI kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa Alhamisi

“Tunahitaji kuimarisha katiba ya mwaka wa 2010. Hatuzungumzii kuhusu kubadilisha katiba bali kuirekebisha, marekebisho ya kwanza kati ya mengi yatakayokuja mbeleni,” akaongeza.

Rais amesema marekebisho hayo kupitia BBI yalisababishwa na msururu wa visa vya ghasia ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa kila baada ya uchaguzi mkuu humu nchini.

Amewakumbusha Wakenya kuhusu hali ilivyokuwa baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 ambapo nchi hii ilishuhudia ghasia na mapigano baina ya jamii yaliyosababisha maafa mengi na watu wengine kupoteza makao yao.

Also Read
KDF yaahidi uwazi na kuepukana na ufisadi kwenye mchakato wa usajili wa makurutu

Kulingana na Rais, pendekezo la kuwepo kwa asilimia 50 ya wanawake katika Bunge la Seneti ni hatua itakayohakikisha kwamba wanawake wanahusika kikamilifu katika kuamua jinsi serikali za kaunti zitafanya matumizi ya migao yao ya rasilimali kutoka kwa serikali kuu.

Hata hivyo, Rais Kenyatta amewahimiza Wakenya kuendelea kuzingatia kanuni za kuzuia maambukizi ya COVID-19 wakati wakiendelea kujihusisha kwenye mchakato huo.

  

Latest posts

Mama Taifa ampongeza Jim Nyamu kwa juhudi zake za kuwatunza Ndovu

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,335 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Nyumba za thamani ya shilingi milioni 10 zabomolewa Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi