Zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Poli katika kaunti 13 kuanza mwishoni mwa wiki

Wadau wa sekta ya afya katika eneo la Mwingi, Kaunti ya Kitui, wameandaa mkutano katika Hospitali ya Mwingi Level 4 ili kujadili zoezi la utoaji chanjo dhidi ya Polio linalitarajiwa kuanza tarehe 22 mwezi Mei mwaka huu.

Mkutano huo ulioongozwa na Afisa wa Afya ya Umma wa Kaunti Ndogo ya Mwingi, Joseph Kimwele, ulinuia kujadili matayarisho ya zoezi hilo.

Miongoni mwa wadau wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, serikali kuu, viongozi wa dini na waandishi wa habari.

Also Read
Jamii ya Wamaasai yahimizwa kuwaandaa watoto wao kwa ufunguzi wa shule

wamejadili kwa kina maelezo kuhusu maradhi ya polio, chanjo dhidi yake, umuhimu wa zoezi hilo la utoaji chanjo, muda wa zoezi hilo na majukumu yatakayotekelezwa na wadau hao mbali mbali.

Zoezi hilo linalenga kuwafikia watoto wengi zaidi katika muda mfupi zaidi, katika juhudi za kuangamiza maradhi hayo ulimwenguni.

Also Read
Maafisa 150,000 wa polisi kudumisha usalama kote nchini wakati wa Uchaguzi Mkuu

Kimwele amefichua kwamba zoezi hilo litaandaliwa katika kaunti 13 humu nchini zilizo hatarini zaidi kati ya tarehe 22 hadi 26 mwezi huu wa Mei.

Kaunti hizo za Nairobi, Kiambu, Kilifi, Mombasa, Mandera, Garissa, Kajiado, Machakos, Wajir, Kitui, Taita Taveta, Isiolo na Lamu ni zile ambazo zimepakana na eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya ambako kisa cha maradhi ya polio kiliripotiwa mwanzoni mwa mwaka huu.

Also Read
Ruto awasuta wanaopinga mfumo wake wa kiuchumi

Afisa huyo pia ameeleza umuhimu wa kusisitiza tofauti kati ya chanjo hiyo ya polio na ile ya Korona ili kuzuia uwezekano wa watu kususia zoezi hilo.

Aidha, Kimwele amehakikisha kwamba wakati wa zoezi hilo, kanuni zote za kuzuia msambao wa virusi vya korona zitazingatiwa.

  

Latest posts

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Maafisa wa Utawala waonywa dhidi ya kujihusisha na siasa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi