Zuchu amnunulia mamake gari

Mwanamuziki wa kampuni ya muziki ya WCB nchini Tanzania Zuchu amemnunulia mamake gari.

Zuchu alitangaza hayo Kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo alipachika video ambayo inaonyesha akimkabidhi mamake Khadija Kopa gari hilo aina ya Toyota Alphard la rangi nyeupe.

Mwanzo wa video hiyo amepachika video ya awali wakiwa ndani ya gari kama hilo huku akikiri jinsi anapenda aina hiyo ya magari.

Also Read
"Siwezi kutafutia Diamond mke!" asema Shilole

Khadija Kopa ambaye pia ni mwanamuziki anasikika akimshukuru mwanawe huku akimwombea dua kwamba ajaliwe vingi maishani.

Khadija Kopa na mwanawe Zuchu

Nyota huyo ambaye anakua kwa haraka katika fani ya muziki chini ya WCB alielezea jinsi hangeweza kumpa chochote mamake mzazi mwaka mmoja uliopita ila sasa anaweza hata kumnunulia gari alipendalo.

Also Read
Wasafi Tv kurejea mwisho wa mwezi!

Zuchu alifichuliwa rasmi na kampuni ya Diamond Platnumz ya Wasafi Classic Baby mwezi wa nne mwaka 2020 na katika kipindi cha mwaka mmoja tu ameafikia ufanisi kimuziki.

Yeye ndiye mwanamuziki wa pili wa kike katika kampuni hiyo ya WCB baada ya Queen Darleen.

Haya yanajiri wakati ambapo binti huyo ametoa kibao kipya kwa jina “Nyumba Ndogo” ambacho kimezua minong’ono so haba huko bongo.

Also Read
Mazishi ya Mighty Salim

Kwenye wimbo huo sauti iliyopo ni ya mke wa pili ambaye anajitambulisha kwa mke wa kwanza huku akimwelezea anayoyafanya ambayo hayamridhishi mume wao.

Kibao cha Zuchu sukari kilifanya vyema zaidi na inaaminika hiki cha nyumba Ndogo cha mtindo wa singeli pia kitafanya vizuri.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi