Zuchu Asema Yuko Tayari Kwa Mapenzi

Zuhura Othman Soud mwanamuziki wa Tanzania maarufu kama Zuchu amesema kwamba Sasa yuko tayari kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Akizungumza kwenye kipindi cha Big Sunday Live, mwimbaji huyo wa kibao ‘Sukari’ alisema amechoka kuulizwa kuhusu mpenzi kila mara na ndio maana ameamua kutafuta.

Zuchu wa umri wa miaka 27 sasa anasema angependa kuanza na urafiki kabla ya uhusiano kugeuka na kuwa wa kimapenzi.

Also Read
Emanuella ashinda tuzo la Nickelodeon

Alisema pia kwamba hana vigezo vingi anapotafuta mpenzi lakini hawezi kutaka mwanaume ambaye ana harufu mbaya ya mwili.

Kando na swala la mpenzi mwanamuziki huyo pia alizungumza kuhusu maswala mengine kama like la kukataa mkataba wa pesa nyingi wa kutangaza pombe. Kulingana naye, dini yake haingemruhusu kutangaza pombe na mamake pia alimshauri asitangaze vileo.

Also Read
Nick Mutuma, Martha Karua,  washerehekea siku ya kuzaliwa

Malkia huyo wa kampuni ya kusimamia wanamuziki ya Wasafi WCB, alijitetea pia dhidi ya madai kwamba anatumia ushirikina kuafikia ufanisi katika muziki. Alisema ufanisi wake kama mwanamuziki unatoka kwa mwenyezi Mungu.

Zuchu amekuwa katika ulingo wa muziki chini ya WCB kwa muda wa mwaka mmoja na miezi kama mitano hivi.

Also Read
Cheche za Zuchu na Diamond zi wapi?

Alitambulishwa rasmi na kampuni ya kusimamia wanamuziki ya Wasafi WCB mwezi Aprili mwaka 2020 na tangu wakati huo nyota yake imekuwa iking’aa.

Vibao vyake vya kwanza kabisa ambavyo ni “Cheche” na “litawachoma” alimshirikisha Diamond Platnumz.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi