Zuchu awapa usaidizi wanawake Zanzibar

Mwanamuziki wa kampuni ya WCB nchini Tanzania Zuchu amekuwepo kwenye ulingo wa muziki kwa muda mfupi ambapo anafanya vyema na tayari ameanza kusaidia jamii kutokana na alichojaliwa.

Jana Alhamisi tarehe mosi mwezi Julai mwaka 2021, binti huyo na mamake Khadija Kopa walifika katika eneo la Zanzibar Mji Mpya wa Kwahani Kibanda Hatari ambapo walilakiwa na Meya wa eneo hilo na kuandaa mkutano na kina mama.

Also Read
Cardi B Ajifungua

Kina mama walionekana kupanga foleni na mmoja baada ya mwingine Zuchu akawakabidhi bahasha isijulikane alikuwa amewawekea pesa ngapi ndani. Wapo ambao hawangefika alikokuwa lakini Zuchu alijitwika jukumu la kuwafikia mwenyewe.

Mwanamuziki huyo anasema msemo kwamba umasikini una sura ya mwanamke humuumiza na ndiposa aliamua kuchukua hatua ya kupunguza umasikini kati ya kina mama nyumbani kwao alikozaliwa Zanzibar.

Also Read
Wanamziki wapya kwenye Konde Gang ya Harmonize

Ana matumaini ya kuweza kuendelea na mpango huo katika sehemu nyingine siku zijazo huku akisema kwamba amejawa na amani na furaha moyoni tangu atimize jambo la jana.

Viongozi waliohudhuria mkutano wa Zuchu walimhimiza aendeleze usaidizi huo kwa kina mama Zanzibar na hata Tanzania nzima siku zijazo.

Zuchu kwa jina halisi Zuhura Othman Soud alitambulishwa rasmi na WCB mwezi Aprili mwaka 2020 na katika muda huo mfupi ameafikia mengi. Alituzwa na mtandao wa YouTube kwa kufikisha wafuasi laki moja kwa muda wa wiki moja tu na baada ya miezi 11 wafuasi hao wakagonga milioni moja.

Also Read
Diamond amsifia Rayvanny

Kando na muziki anafanya kazi za ubalozi kama vile balozi wa Utalii Zanzibar na pia ni balozi wa kamouni kadhaa ikiwemo kampuni ya Zantel kati ya nyingine nyingi.

  

Latest posts

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Kibao Kipya cha Ringtone na Rose Muhando

Marion Bosire

Mulamwah Akaribisha Mwanawe

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi