Zuchu Kutumbuiza Kwenye Mkutano Mkuu wa Mashabiki wa Timu ya Simba

Timu ya mpira wa miguu nchini Tanzania Simba inajiandaa kwa siku yake kuu hapo kesho tarehe 8 mwezi wa nane katika uwanja wa michezo wa Benjamin Mkapa wilayani Temeke jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Msanii wa muziki nchini humo Zuhura Othman maarufu kama Zuchu ni mmoja wa wasanii ambao watatumbuiza mashabiki hao na amesema kwamba anawaandalia onyesho la kipekee.

Also Read
Wakenya Joash Onyango na Francis Kahata wazidi kuandikisha historia na Simba SC

Akizungumza kwenye mahojiano kuhusu siku hiyo, Zuchu alisema kwamba anaandaa tamasha la kipekee kutokana na pesa nyingi ambazo amelipwa na usimamizi wa timu hiyo. Mwanamuziki huyo alifafanua kwamba ubora wa onyesho la msanii jukwaani unaamuliwa na kiasi cha pesa ambazo amelipwa. Ikiwa amelipwa nyingi basi ataridhisha na akilipwa kidogo basi hatajituma sana. Kulingana naye, wanamuziki huwekeza kiasi kikubwa sana cha fedha kwenye kunakili sauti ya nyimbo zao pamoja na video ndiposa wanahitaji kulipwa vizuri.

Also Read
Mzozo Kati ya Mo'Nique na Netflix Wasuluhishwa

Binti huyo wa mwimbaji maarufu wa Taarab Khadija Kopa anasema amekuwa akifanya mazoezi kuanzia tarehe 30 mwezi jana kujiandaa kwa siku ya Simba. “Ninataka onyesho hilo liwakilishe jina langu kama msanii, jina la kampuni yangu WCB na ukubwa wa timu ya Simba.” alisema Zuchu.

Also Read
"Tushirikishe, msifunge mikutano ya ibada!" Faustin Munishi

Timu ya Yanga ambayo ndiyo mshindani mkuu wa Simba kwenye soka ya Tanzania iliandaa hafla sawia jana tarehe 6 mwezi Agosti.

  

Latest posts

Gravity Awataka Bebe Cool na Jose Chameleone Wastaafu

Marion Bosire

Kibao kipya cha Nonini kuzinduliwa siku ya kuzaliwa kwake

Tom Mathinji

Brenda Jons atangaza kuwa sasa ameokoka

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi